News

NDUGAI AFUNGUA MAONESHO WIZARA YA MADINI NA TAASISI ZAKE DODOMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo tarehe 26 Mei, 2019 amefungua maonesho ya siku mbili ya Wizara ya Madini pamoja na taasisi zake yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini

Dodoma. Taasisi zinazoshiriki ni pamoja na Tume ya Madini, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC). Wadau wengine wanaoshiriki katika maonesho hayo ni pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), TAMIDA, kampuni za madini pamoja na asasi za kiraia.

Lengo la maonesho hayo lilikuwa ni kuelimisha wabunge ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020 unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Mei, 2019

Mbali na kupongeza maandalizi yaliyofanywa na Wizara ya Madini na taasisi zake, Ndugai ameitaka Wizara kuendelea kuelimisha umma na kutangaza fursa kwenye Sekta ya Madini ili Sekta ya Madini iwe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.

 

SOURCE BY: TANSHEQ LIMITED